Download Mp3 | Harmonize - Namba Moja | New Song Audio

Download Mp3 | Harmonize – Namba Moja | New Song Audio 
[Verse 1] 
Uwezo sina, n’ngalin’jengea nyumba
Uuh nyumba, uwenda angekubali
Pia sauti sina, n’ngali muimbia rhumba
Uhh rhumba, ili asiende mbali
Nimenaswa na ulimbo, tena ni maji ya shingo
Nyuma nyuma ka mgambo, natamani nimwambie
Mi naogopa michambo, najipa moyo mawindo
Niisute ya pendo, mi nataka niwe nae
[Pre-Chorus]
Hata waniite zoba, waseme ameniroga
Kumuacha ndo siwezi, nimeridhia
Ye ndie namba moja, wengine watangoja
Kusema ndo siwezi, mi naumia
[Chorus]
Pale napomuona
Mwa ndelele, mwa ndelele, mwa ndelele
Jamani moyo
Mwa ndelele, mwa ndelele, mwa ndelele
Pale napomuona
Mwa ndelele, mwa ndelele, mwa ndelele
Yarabi moyo
Mwa ndelele, mwa ndelele, mwa ndelele
[Verse 2]
Ishara Mungu alikuumba, kwa udongo mchanga
Nikufanyie ndumba, uh na ukanizimia
Nikusanye waganga, Zanzibar na Tanga
Wahodari wa nyanga, bado nafikiria
Macho yangu hachoki mtizama
Ukiwa mbali nami, moyo unalipuka (ayaya!)
Tatizo langu nashindwa kusema
Hivi kisa nini moyo unateseka?
Nimenaswa na ulimbo, tena ni maji ya shingo
Nyuma nyuma ka mgambo, natamani nimwambie
Mi naogopa michambo, najipa moyo mawindo
Niisute ya pendo, mi nataka niwe nae
[Pre-Chorus]
Hata waniite zoba, waseme ameniroga
Kumuacha ndo siwezi, nimeridhia
Ye ndie namba moja, wengine watangoja
Kusema ndo siwezi, mi naumia
[Chorus]
Pale napomuona
Mwa ndelele, mwa ndelele, mwa ndelele
Jamani moyo
Mwa ndelele, mwa ndelele, mwa ndelele
Pale napomuona
Mwa ndelele, mwa ndelele, mwa ndelele
Yarabi moyo
Mwa ndelele, mwa ndelele, mwa ndelele
[Outro]
Mi nitaringa, ntaringa na yeye, ntaringaje!
(Nikiwa nae)
Ntaringa, ntaringa na yeye, ntaringaje!
(Nikimpata oh oh)
Mi nitaringa, ntaringa na yeye, ntaringaje!
(Nitaringa nae)
Mi nitaringa, ntaringa na yeye, ntaringaje!
(Nitaringa nae)
Mi nitaringa, ntaringa na yeye, ntaringaje!
(Nitaringa nae)
Mi nitaringa, ntaringa na yeye, ntaringaje!
(Nikiwa naye)
Na Sheddy Clever
Ntaringa, ntaringa na yeye, ntaringaje!
Mi nitaringa, ntaringa na yeye, ntaringaje!
Harmonize baby!
https://goo.gl/RD5aBF
https://www.mpyakali.com/p/blog-page_24.html SHARE WITH FRIENDS
Share on Google Plus
    Leave Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment